Home Habari za michezo HUKU KANUNI MPYA ZA LIGI KUU ZIKIWA ZINAPENDELEA MASTAA WA NNJE...

HUKU KANUNI MPYA ZA LIGI KUU ZIKIWA ZINAPENDELEA MASTAA WA NNJE TU…KIBU DENIS ANG’ATA MENO KWA HASIRA…


Ongezeko la wachezaji wa kigeni kutumika wote 12 katika mchezo mmoja kutoka nane ni jambo ambalo limewapa presha wazawa wengi kupata nafasi ya kucheza lakini hali hiyo imekuwa tofauti kwa mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis anayeamini ataendelea kukiwasha.

Simba msimu huu imesajili wachezaji wapya wanane wazawa wawili Nassor Kapama na Habib Kyombo huku wageni wakiwa ni sita ambao ni Mohamed Ouattara, Victor Akpan, Nelson Okwa, Moses Phiri, Augustine Okrah na Dejan Georgijevic na sita kati ya hao wote ni viungo washambuliaji ambao wanawania namba na Kibu lakini mwenyewe hawazi.

Akizungumza nyota huyo wa zamani wa Mbeya City, Geita Gold na Kumuyange FC ameeleza; “Timu imebadilika tofauti na msimu uliopita, tumeimarika zaidi na wachezaji wapya walioongezeka wameleta ushindani zaidi wa namba jambo ambalo ni zuri kwa timu.”

“Kwa upande wangu sioni shida kwani najiamini nina uwezo mkubwa wa kucheza huku nikizingatia maelekezo ya makocha hivyo namuachia kocha ndiye ataamua ampange nani na kwenye mechi gani.”

Simba hadi sasa ina wachezaji wa kigeni 12 na safu ya ushambuliaji na winga ambayo anacheza Kibu wapo 11 ambao ni Phiri, Okwa, Okrah, Dejan, Peter Banda, Pape Sakho, Clatous Chama na wazawa John Bocco, Habib Kyombo, Jimmyson Mwanuke na Kiraka Kapama wote wanawania namba.

Pamoja na ushindani huo, Kibu ameonekana kumkosha kocha mpya Zoran Maki na amempanga katika kikosi cha kwanza kwenye mechi mbili, ile ya Simba Day dhidi ya St George ya Ethiopia na kufunga bao la kwanza katika ushindi wa mabao 2-0, na ile ya Ngao ya Jamii, Simba ikilala mabao 2-1 mbele ya watani zao Yanga.

Simba itarusha karata yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Mkapa dhidi ya Geita Gold kuanzia saa 1:00 usiku.

Ni mechi ngumu ambayo Maki ameahidi kuja kivingine kabisa baada ya kupoteza dhidi ya Yanga wikiendi iliyopita.

SOMA NA HII  BREAKING NEWS : KOCHA WA YANGA AFARIKI DUNIA