Home Habari za michezo HUU HAPA UKWELI WA KAGERE KUSAJILIWA SINGIDA BIG STAR…PLUIJM NAYE NDANI YA...

HUU HAPA UKWELI WA KAGERE KUSAJILIWA SINGIDA BIG STAR…PLUIJM NAYE NDANI YA NYUMBA….


Taarifa za ndani kabisa zinaeleza kuwa, kuna uwezekano mkubwa leo Singida Big Star wakamtambulisha Meddie Kagere kuwa jembe lao jipya kwa ajili ya kuelekea kwenye mapambano ya Ligi Kuu 2022-23.

Imeelezwa kuwa, Singida Big Stars imeshakamilisha usajili na baada ya kusaini, amepewa ruksa ya siku kadhaa kurejea kwao Rwanda na kisha kurejea tena nchini kujiunga na matajiri hao wa Singida.

Akizungumza na Wasafi FM asubuhi ya leo, msemaji wa Singida Big Star, Dismas Ten, alisema wana sapraiz kubwa leo katika tamasha lao la kutambulisha wachezaji ambalo pia litahusisha mechi kati ya Singinda Big Star dhidi ya Zanaco ya Zambia.

“Tunayo sapraiz ambayo mashabiki wataiona hapo baadaye uwanjani. Kuhusu Kagere ni mchezaji mzuri, lakini ibaki kama nilivyokwambia sisi tunayo sapraiz hapo baadaye,” alisema Ten.

Kwenye ukurasa wao wa Instagram, Singida Big Star tayari wameweka picha za wachezaji wakiingia uwanjani na basi lao huku pia akionekana aliyekuwa kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm ambaye amekula kandarasi ya kuwanoa matajiri hao wa Singida.

SOMA NA HII  SINGIDA BIG STARS WAONYESHA JEURI YA PESA....BAADA YA KUMRUDISHA KOCHA HANS PLUIJM...WAMVUTA NA PASCAL WAWA...