Home Habari za michezo IMETIKI…..BAADA YA KUSUSWA NA TIMU ZA BONGO….KABWILI APATA TIMU RWANDA….MCHONGO MZIMA KAZE...

IMETIKI…..BAADA YA KUSUSWA NA TIMU ZA BONGO….KABWILI APATA TIMU RWANDA….MCHONGO MZIMA KAZE ANAUJUA…


Aliyekuwa kipa wa Yanga, Ramadhan Kabwili amejiunga rasmi na Klabu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Kabwili ambaye alimaliza mkataba wake na Yanga, amekamilisha dili hilo huku ikielezwa kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze akihusika.

Timu hiyo ambayo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya nne inahitaji kurejesha heshima kwenye soka la nchi hiyo huku ikiamini usajili wa kipa huyo utawasaidia kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Kabwili aliyewika na Serengeti Boys iliyoshiriki AFCON ya vijana 2017 nchini Gabon alipendekezwa na kocha wa makipa wa timu hiyo Mrundi, Vladimir Niyonkuru aliyewahi kufanya kazi nae ndani ya Yanga miaka kadhaa nyuma.

Kipa huyo alianzia Akademi ya Azam kisha kuhamia Yanga alipokaa kwa miaka mitano kabla ya kumaliza mkataba wake msimu huu.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA JUMAMOSI HII...SURE BOY 'AMNG'ATA SIKIO' NABI....ALILIA KUKIVURUGA PALE KATI...