Home Habari za michezo KISA KUSHIRIKI AFCON….KLABU YA NAPOLI YA ITALI WAKATAA KUSAJILI MCHEZAJI KUTOKA AFRIKA…WAPIGA...

KISA KUSHIRIKI AFCON….KLABU YA NAPOLI YA ITALI WAKATAA KUSAJILI MCHEZAJI KUTOKA AFRIKA…WAPIGA MKWARA HASWA…

 


Rais wa Klabu ya Napoli nchini Italia, Aurelio De Laurentiis ametangaza kwamba katika siku zijazo hatokubali klabu yake kuwasajili wachezaji kutoka mataifa ya Afrika.

Aurelio amesema kwamba klabu ya Napoli itakuwa ikiwasajili wachezaji kutoka Afrika iwapo tu watakubali masharti ya kuacha kutumikia timu zao za Taifa katika mashindano ya AFCON.

“Niliwaambiwa wasiniambie tena kuhusu Waafrika. Mimi nawapenda, lakini iwapo watakula kiapo kwa njia ya maandishi kwamba hawatoshiriki katika michauno ya AFCON ama mashindano kama kufuzu mashindano ya ubingwa wa dunia kule Amerika ya Kusini, wachezaji hawa huwa hawapatikani,” Rais Aurelio amesema.

Aliongeza kuwa Klabu ya Napoli ndio wajinga wa kuendelea kuwalipa mishahara minono ya kuwawezesha kusafiri kote duniani kuwajibikia mataifa yao katika mashindano mbalimbali.

Itakumbukwa kwamba katika kipute cha AFCON mwaka 2021 amabcho kilipigwa mwezi Januri-Februari, na Senegali ilitwaa Ubingwa. Klabu ya Napoli ilitishia kushtaki mataifa ya Afrika ambayo yalikuwa yakiwataka wachezaji wake kuyawakilisha kutoka klabu hiyo. Wachezaji hao walikuwa ni mshambuliaji Victor Osimhen kutoka Nigeria, beki Kalidou Koulibaly kutoka Senegal, Anguissa Andre Zambo na wengine.

Taarifa hizi bila shaka zitawaathiri sana wachezaji wengi wa Kiafrika waliokuwa na ndoto ya kuisakatia klabu hiyo ya Italia huku pia wachezaji kama Victor Osimhen na Anguissa Zambo ambao bado wanaichezea klabu hiyo wakiwa katika hali ya sintofahamu kutokana na taarifa hiyo ya rais wa klabu.

SOMA NA HII  KUPANGA NI KUCHAGUA...KAMATA NJIA RAHISI YA KUPUNA MAPENE NDANI YA KASINO YA MERIDIANBET...