Home news TANZIA: MCHEZA KIKAPU CHIPUKIZI AFARIKI

TANZIA: MCHEZA KIKAPU CHIPUKIZI AFARIKI


 MCHEZA kikapu chipukizi kutoka chuo kikuu cha mchezo wa mpira wa kikapu cha Kentucky kilichopo nchini Marekani, Terrence Clarke amefariki Dunia baada ya kupata ya ajali ya gari iliyotokea kwenye jiji la Los Angeles nchini Marekani.

 

 Clarke aliyefariki akiwa na umri wa miaka 19, mwenye urefu wa futi 6 na inchi 7 alikuwa anatajwa kuwa miongoni mwa wacheza kikapu bora chipukizi tena kutoka kwenye nafasi ya ulinzi tokea mwaka 2020 jambo ambalo limewagusa mashabiki wengi wa mchezo huo Duniani.

 

Baada ya kifo kutangazwa, aliyekuwa kocha wake, John Calipari amesema; “Wote tupo kwenye mshangao mkubwa. Hiki kitakuwa kipindi kigumu kwa wote waliomfahamu na kumpenda Terrence, na nimuombe kila mmoja achukue wasaa kumuombea Terrence na familia yake. Apumzike kwa amani”.

 

Terrence ambaye alikuwa na ndoto ya kucheza NBA, mwezi uliopita alisaini mkataba wa kuendelea kucheza ligi hiyo ambapo aliambulia kucheza michezo 8 tu ya msimu uliopita baada ya kusumbuliwa na majeraha kwenye mguu wake wa kulia.


SOMA NA HII  KIPA MBRAZIL WA SIMBA ATAKIWA KUTHIBITISHA UBORA WAKE, KIPA WA MAKOCHA AFUNGUKA KILA KITU, MANULA ATAJWA