Home Simba SC CHAMA YEYE NI MZEE WA REKODI, MECHI ZAKE NA MABAO ACHA KABISA

CHAMA YEYE NI MZEE WA REKODI, MECHI ZAKE NA MABAO ACHA KABISA


TANGU ajiunge na timu ya Simba, Septemba 15, 2019, Clatous 
Chama raia wa Zambia amecheza jumla ya michezo 112, na kuwa na mchango mkubwa katika kikosi hicho.

Kiungo huyo mchezeshaji amekuwa na umuhimu mkubwa katika kikosi cha Simba kuanzia katika michuano ya ndani ya Tanzania na ile ya Kimataifa, akiwa msaada katika kubeba mataji ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

Ana jumla ya pasi za mwisho 45 tangu ajiunge na kikosi cha Simba hiyo ni kwenye mashindano yote akitokea Power Dynamos ya Zambia.

Kwa msimu huu mpaka sasa katika Ligi Kuu Bara, Chama ameshafikisha jumla ya asisti 11 na bado zimesalia mechi za kuendelea kuchezwa kwa Simba na ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Didier Gomes.

Katika mabao Chama amefunga jumla ya mabao 30 kwenye michezo yote ikiwemo ile ya Ligi ya Mabingwa ambayo kwa msimu huu Simba imeingia hatua ya robo fainali.

SOMA NA HII  MANGUNGU MINNE TENA SIMBA....AIBUKA NA USHINDI WA KISHINDO ...ASHA BARAKA KAMA KAWA....