Home news NJOMBE MJI YAPIGWA TAFU KIMTINDO NA BOSI

NJOMBE MJI YAPIGWA TAFU KIMTINDO NA BOSI

 


BOSI wa Yanga, ambaye ni Mjumbe wa Kudumu wa Heshima 
ndani ya klabu hiyo, Thobias Lingalangala ameiongezea nguvu timu ya Njombe Mji ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa msimu huu.

Njombe Mji ilishiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 na kushuka daraja kwa msimu huo baada ya kushika nafasi ya 16 na kukusanya pointi 22.

Kwa sasa ipo Kundi A ikipambana kujinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja.

 Lingalangala amesema kuwa:“Kwa sasa naisaidia timu ya Njombe Mji kwa ajili ya kuhakikisha inapanda daraja kwa msimu huu, ni timu ya nyumbani, japo mambo yanazidi kuwa magumu lakini tuna imani kwenye michezo iliyobaki watafanya vizuri.”

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 8 imekusanya pointi 16 baada ya kucheza mechi 14 huku Boma FC tayari imeshakata tamaa ya kubaki Ligi Daraja la Kwanza kwa kuwa ina pointi 6 baada ya kucheza mechi 14.

SOMA NA HII  BAADA YA KUWATEMA PABLO NA MORRISON...MO DEWJI ABARIKI CHAMA NA MASTAA HAWA10 KUPIGWA CHINI SIMBA...