Home Habari za michezo KISA SIMBA KUITWA ‘MAKOLO’…OSCAR OSCAR AFURA KWA MANENO NA KUMSHUKIA MANARA JUMLA...

KISA SIMBA KUITWA ‘MAKOLO’…OSCAR OSCAR AFURA KWA MANENO NA KUMSHUKIA MANARA JUMLA JUMLA…


Mchambuzi nguli wa masuala ya Soka nchini, Oscar Oscar ‘Mzee wa kaliuwa’ ameonyesha kutofurahishwa na kitendo cha aliyewahi kuwa Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara kuwapa jina la utani la ‘Makolo’ klabu yake hiyo ya zamani.

Akizungumza katika kipindi cha Jioni ya Leo kinachoruka kupitia E-Radio kuhusu Manara kutimiza mwaka mmoja baada ya kuhamia Yanga, Oscar amesema licha ya kuwepo majina mengi ya utani, lakini ‘Makolo’ ni jina baya ambalo yeye hapendi hata kulisikia.

“Kitu ambacho sikukipenda kwenye move ya Haji Manara kutoka Simba kwenda Yanga ni kufika na kuwaita Simba ‘Makolo’. Nadhani ni moja ya majina ninayoyachukia sana, na Haji amekuwa muasisi wake.

“Hata kama ni utani lakini kama kuna kitu nilikichukia kwenye move ya Haji, ni kuwaita Simba Makolo. Likolo hata hujui ni li kitu gani ambalo linazungumzwa, naliona ni li kitu tu ambalo halina mpango wowote, nadhani hiyo haikuwa nzuri.

“Haji lazima awe na heshima…. Lakini katika maneno yote na utani wote wa Simba na Yanga ambao wametaniana, hii Kolo imekaa vibaya, hii inasumbua sana haijakaa vizuri, anatakiwa awe na heshima,” amesema Osacr.

SOMA NA HII  HIZI HAPA 'MASHINE NANE ZA KIMATAIFA' ZINAZOIPIGANIA HESHIMA YA BENDERA YA TANZANIA...

1 COMMENT