Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI DHIDI YA UGANDA…KOCHA TAIFA STARS ATAMBA KUANDAA ‘PILIPILI KICHAA’ NYINGI...

KUELEKEA MECHI DHIDI YA UGANDA…KOCHA TAIFA STARS ATAMBA KUANDAA ‘PILIPILI KICHAA’ NYINGI ZA USHINDI….


Kocha Mkuu wa Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen amesema atautumia muda wa siku sita uliosalia kukiandaa Kikosi chake kabla ya kuikabili Uganda ‘The Cranes’ mwishoni mwa juma hili.

Stars itacheza nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam katika mchezo huo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’ zitakazounguruma mapema mwaka 2023 nchini Algeria.

Kocha Pulsen amesema kikosi chake kinaanza kambi leo Jumatatu (Agosti 22) jijini Dar es salaam, baada ya kutaja kikosi mwishoni mwa juma lililopita na ana mataraji makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

Amesema muda uliobaki hautoi nafasi kwa kikosi chake kucheza mchezo wa Kirafiki, lakini atautumia kukiandaa kwa mbinu mbalimbali ili kufanikisha kinachokusudiwa kwenye mchezo huo wa mkondo wa kwanza kabla ya ule wa pili utakaopigwa Uganda juma lijalo.

“Ili tuendelee kuwa na matumaini ya kucheza ‘CHAN’ lazima tushinde dhidi ya Uganda. Tuna siku chache za maandalizi, ambazo hazitoshi kutupa mchezo wa kirafiki lakini tutazitumia vizuri kuhakikisha tunakuwa bora.” amesema Kocha huyo kutoka Denmark

Stars ilianza Kampeni ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN 2023’ kwa kuibanjua Somalia kwa jumla ya mabao 3-1.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA KUSEPA TENA SIMBA....CHAMA AVUNJA UKIMYA..."UONGOZI UFANYE MAAMUZI...NITAANZA MAISHA MENGINE"...