Home Habari za michezo MFAHAMU STAA MKUBWA WA SOKA DUNIAN ANAYELIPWA BILION 26 LAKINI BADO ANAISHI...

MFAHAMU STAA MKUBWA WA SOKA DUNIAN ANAYELIPWA BILION 26 LAKINI BADO ANAISHI KWA WAZAZI WAKE…


Kikawaida ni kwamba Kijana wa miaka 23 anayeingiza sio chini ya bilioni 26 kwa mwaka wengi watategemea kwa utajiri huo awe ni Mtu anayejitegemea na anayeishi kwenye Jumba lake moja kali kivyakevyake na sio kukaa na Wazazi ila kwa Mchezaji wa Liverpool Trent Alexander-Arnold kwake ni tofauti.

Katika umri wa miaka 23 Trent ameshapata mafanikio makubwa kama vile kutwaa kombe la ligi kuu la Uingereza, Ligi ya Mabingwa, Kombe la FA, Uefa Super Cup na kombe la dunia la vilabu ya FIFA na hata mkwanja anaolipwa hapo Liverpool sio chini ya Bilioni 26 TSH kwa mwaka lakini bado anaishi na Wazazi wake nyumbani kwao na kuendelea kufanya kazi kama kama kusaidia kuosha vyombo na kuishi kama Mtu mwenye kipato cha kawaida sana.

“Siku zote nadhani Wachezaji wachanga wanaharakisha mambo, wakianza kulipwa pesa huwa wanafikiria jambo la kwanza kupata gari jipya au kuhama nyumbani alafu unakokwenda kukaa ni mazingira mapya lakini ukiishi nyumbani na Wazazi wako ni tofauti na wanakusaidia kwa mambo mengi, sijawahi kuwa na haraka ya kuhama home” alisema Trent.

SOMA NA HII  VITA VYA UKRAINE VYAMFANYA STRAIKA KUTAFUTA TIMU YA KUCHEZA BONGO...FIFA WAMPA BARAKA ZOTE...