Home Habari za michezo ISHU YA JEZI MPYA …SIMBA WAIBUKA NA HOJA HII TENA..WATAJA MUDA NA...

ISHU YA JEZI MPYA …SIMBA WAIBUKA NA HOJA HII TENA..WATAJA MUDA NA MAHALI ZITAKAPOPATIKANA…


Baada ya sintofahamu ya siku kadhaa kuhusiana na suala la Jezi mpya za Msimu 2022/23 za wekundu wa Msimbazi Simba kuelekea kilele cha Tamasha la Simba Day, hatimaye kitendawili hicho kinateguliwa leo Agost 7, majira ya saa tano asubuhi.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Klabu ya Simba imetoa taarifa inauomaliza maswali yote yanayohusiana na jezi mpya ya msimu wa 2022/23.

Simba SC imeandika;

“Jezi bora kuanzia ubunifu hadi namna ilivyotengenezwa imefika. Hii haijawahi kutokea Afrika Mashariki na Kati.

Saa 5:00 asubuhi tutazindua jezi na muda huo zitaanza kuuzwa kwenye duka la Vunja Bei Sinza Madukani”.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA NAMUNGO FC HIKI HAPA