Home Simba SC NYOTA NANE WA SIMBA HATIHATI KUWAKOSA WAARABU

NYOTA NANE WA SIMBA HATIHATI KUWAKOSA WAARABU


  
DIDIER Gomes huenda akawakosa nyota wake nane kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Waarabu wa Misri, Al Ahly utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Februari 23.

Nyota hao ambao kwa ujumla wamehusika kwenye mabao 12 kwenye Ligi Kuu Bara kati ya 42 yalifungwa na Simba.

Mshambuliaji mzawa namba moja, John Bocco ambaye  ana mabao 8 na pasi mbili za mabao hajawa fiti kwa kuwa anasumbuliwa na majeraha licha ya kuanza mazoezi.

 Perfect Chikwende ingizo jipya ndani ya Simba, kutoka FC Platinum akiwa ametoa pasi ya bao moja mbele ya Dodoma Jiji hayupo kwenye mpango wa mechi za kimataifa.

Nyota sita wa kikosi cha Simba ambao waliachwa Congo na timu ilipokwenda kuwatungua bao 1-0 AS Vita kutokana na kile ambacho kimeelezwa kuwa mamlaka ya Congo iliwataka wabaki huko kwa kwa uangalizi maalumu kwa madai kwamba wana Virusi vya Corona bado hawajawa fiti pia.

Nyota hao ni kipa namba tatu, Ally Salim,Kenedy Juma, Erasto Nyoni ambaye ni beki kiraka, kiungo Rarry Bwaly yeye ana asisti 1 aliitoa mbele ya JKT Tanzania, beki wa kati Ibrahim Amen na kiungo mkabaji Jonas Mkude.

Pia walibaki huko na meneja wa Simba, Abas Seleman ambao walibaki nchini Congo ila kwa sasa wote wamerejea na wameanza na majukumu ndani ya kikosi hicho.

 Ofisa Habari wa Simba Haji Manara alisema kuwa majibu yaliyotoka kwenye maabara ya Congo ya Taifa ilionyesha kuwa kuna baadhi ya wachezaji wana Corona ila walipopima maabara nyingine walisema hawajaadhirika na Corona ndio maana Kenedy Juma na  Rarry Bwalya walicheza.

Kuhusu kurejea kwa nyota hao, Manara alisema kuwa tayari wamesharejea na moja kwa moja waliingia kambini na kuanza mazoezi hivyo wanamuongezea upana kikosi mwalimu ambaye ana kazi ya kupanga kikosi cha ushindi.


SOMA NA HII  MGUNDA AIBUKA NA HAYA MAPYA KUHUSU OKWA NA YANAYOMSIBU..."NILIMUONDOA"...