Home Yanga SC YANGA YATAMBA KUFIKIA REKODI YA SIMBA KAGAME

YANGA YATAMBA KUFIKIA REKODI YA SIMBA KAGAME


KUELEKEA kuanza kutimua vumbi kwa michuano ya kombe la Kagame leo Jumapili, Uongozi wa klabu ya Yanga umetamba kuwa umejipanga vizuri kuhakikisha unaibuka na ubingwa wa michuano hiyo, na kufikia rekodi ya Simba ya kutwaa ubingwa huo mara sita.

Michuano hiyo ambayo inatarajiwa kushirikisha timu nane zilizowekwa kwenye makundi mawili yaani kundi A na B, itaanza kutimua vumbi rasmi leo kwa mchezo mmoja kupigwa kwenye uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Yanga wao watafungua dimba kwa kushuka uwanjani saa 1 usiku, kucheza dhidi ya Big Bullets FC kutokea nchini Malawi.

Akizungumzia mipango yao kwenye michuano hiyo, Ofisa habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema: “Tumekuwa na muda mzuri wa maandalizi ya kikosi chetu kuelekea michuano hii ya CECAFA, na malengo yetu makubwa ni kuibuka mabingwa wa michuano ya mwaka huu.

“Kwa kuwa hii ni michuano mikubwa na inashirikisha timu mbalimbali kutoka nje ya nchi tunatarajia kukutana na ushindani mkubwa, lakini tuna matumaini makubwa ya kutwaa kombe letu la sita mwaka huu.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUIFANIKISHIA KUTINGA ROBO FAINAL CAF....GSM KABAKI NA DENI HILI TU KWA YANGA...