Home Habari za michezo SIMBA vs MTIBWA KESHO NI MECHI YA KUMALIZA UBISHI….CHAMA KUKOSEKANIKA TENA…

SIMBA vs MTIBWA KESHO NI MECHI YA KUMALIZA UBISHI….CHAMA KUKOSEKANIKA TENA…

Habari za Simba SC

SIMBA wanashuka dimbani kesho kujiuliza kwa mara nyingine mbele ya wageni wao, Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi Dar-es-Salaam saa 10:00 alasiri.

Timu zote zinahitaji pointi muhimu ambapo Simba anahitaji kujiweka salama kuwania nafasi ya pili huku Mtibwa Sugar wakihitaji kujiweka katika mazingira mazuri ya mwisho wa msimu kutoshuka daraja.

Mechi tano za mwisho Simba alishinda nne na sare moja mbele ya wakata miwa hao, mchezo wa mzunguko wa kwanza Agosti 17, 2023, Mtibwa Sugar 2 – 4 Simba.

Machi 11, 2023, Mtibwa Sugar 0-3 Simba, Oktoba 30, 2022, Simba 5 -0 na Juni 23, 2023, Simba 2-0 Mtibwa Sugar, Januari 22, 2022 Mtibwa 0 -0 Simba.

Kuelekea mchezo wa leo Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema hii ni ligi hawawezi kuijadili Mtibwa Sugar kwa nafasi waliopo na wanaenda kucheza kwa tahadhari zote kwa sababu ya ugumu wa timu hiyo.

Amesema katika mchezo wa pili kuna makosa na walifanya makosa mechi iliyopita na maandalizi yote ya kucheza na timu ya Mtibwa Sugar yapo vizuri.

“Tutamkosa Chama (Clatous), mchezo wa Leo kutokana na adhabu aliyoipata lakini Simba imefanya usajili wa wachezaji wengi na watapata nafasi ya kucheza na kuonyesha kitu kizuri.

Vijana wapo vizuri wanajua uzito wa mechi hii na umuhimu wake, wachezaji wapo tayari kwa mchezo kuhakikisha tunafanikiwa kupata matokeo mazuri kwa kuvuna pointi tatu muhimu,” amesema Mgunda.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema mechi itakuwa ya ushindani kwa sababu wanakutana na Simba ambayo imetoka kupoteza na wao wanahitaji kupata matokeo.

Amesema wamefanyia kazi mapungufu yao na kusahihisha na wanaenda kukutana na wapinzani wa tahadhari kubwa kwa ajili ya kuvuna alama tatu ambazo zitawasaidia kuwaweka katika nafasi nzuri.

“Unapochsza na Simba haijalishi wanakosa wachezaji gani, hata sisi tunakosa baadhi ya wachezaji tumejipanga na presha ya kutafuta matokeo kama ilivyo kwa wapinzani wetu,” amesema Katwila.

Ameongeza kuwa makosa madogo madogo lazima yapungue yasije kutogalimu lakini wanatakiwa kuwa makini kutumia mapungufu ya Simba ili kutafuta pointi tatu mbele ya wapinzani wao.

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA KUHUSU MASTAA HAWA KUKOSA WAPINZANI KIKOSINI