Home Habari za michezo MANDONGA:- “NAONA WAZI SIMBA IMECHOKA…AFANYA UTABIRI HUU WA MATOKEO

MANDONGA:- “NAONA WAZI SIMBA IMECHOKA…AFANYA UTABIRI HUU WA MATOKEO

MANDONGA:-

Karim Mandonga amefunguka kuwa yeye ni shabiki wa kutupwa wa
Klabu ya Yanga SC na kuelekea mchezo wa Jumamosi dhidi ya Simba Sc kuwa utakuwa mchezo wa rahisi na wa wazi kwa Yanga kupata matokeo.

Yanga na Simba watashuka dimbani Aprili 20, kuvaana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC huku Yanga wakionekana kuwa bora zaidi kulingana na takwimu za misimu takribani miwili ikilinganishwa na Simba.

“Yanga ni timu yangu alafu naipenda sana, sina presha juu ya kupata matokeo ya ushindi mbele ya Simba ambayo naona wazi imechoka kulingana na ubora wa Yanga.

“Angalia namna ambavyo imefanikiwa kufanya makubwa katika Ligi ya mabingwa Afrika na hakuna ambaye alitegemea lakini iliweza kuweka rekodi kubwa sana ndiyo maana naona wazi Simba haiwezi kuchomoka maana tutawafunga mabao 3-0.”

SOMA NA HII  PATRICK AUSSEMS AKIMBIA TIMU KENYA....AISHIA KUWAPA MATUMAINI KWA 'VIDEO CALL'...TIMU YA RWANDA YATAJWA KUHUSIKA...