Home Habari za michezo KAZIER CHIEFS KUMBEBA GAMONDI JANGWANI….MWENYEWE ADAI HANA UHAKIKA NA YANGA…

KAZIER CHIEFS KUMBEBA GAMONDI JANGWANI….MWENYEWE ADAI HANA UHAKIKA NA YANGA…

Habari za Yanga leo

Inaelezwa wakati Yanga ilipokuwa Sauzi ikicheza na Mamelodi Sundowns katika mechi ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, klabu kubwa ya huko Kaizer Chiefs ilikuwa inapiga hesabu ikiwa jukwaani na fasta ikalichukua jina la kocha wa wababe hao wa Ligi Kuu Bara, yaani Miguel Gamondi.

Kaizer Chiefs maarufu kama Amakhosi wameluichukua jina la Gamondi katika mchujo wa mwisho kati yake na kocha wa zamani wa Yanga aliyepo Far Rabat ya Morocco, Nasreddine Nabi aliyebakiza hatua chache kuipa klabu anayoinoa ubingwa wa nchi hiyo maarufu kama Pro Batola.

Taarifa za uhakika kutoka Sauzi, zinasema kuwa awali klabu hiyo ilikuwa imebaki na jina la Nabi pekee ambaye walishaanza hesabu naye kwa muda mrefu tangu alipomaliza mkataba na Yanga na kuondoka Jangwani, lakini dili hilo likabuma baada ya kocha huyo Mtunisia kuamua kutimkia Morocco.

Nabi aligomea ofa ya Kaizer baada ya klabu hiyo kushindwa kukubaliana naye kufuatia kocha huyo kutaka ashuke na benchi la watu watatu hatua ambalo mabosi wa timu hiyo walishindwa kukubaliana nalo kutokana na bajeti waliyokuwa nayo kipindi hicho.

Rekodi tamu alizonazo Nabi ndani ya Rabat akiiwezesha timu hiyo kuongoza msimamo wa Ligi ya Morocco kwa kushinda mechi 16 mfululizo kati ya 18 ilizoshinda zimeifanya Kaizer kumfikiria kocha huyo ili kwenda kuokoa jahazi la timu hiyo.

Lakini, ghafla baada ya Yanga kutua Sauzi na Gamondi na kushusha sapraizi bab’kubwa ya kuwabana Mamelodi nyumbani baada ya awali kuwabana Kwa Mkapa iliwashtua mabosi wa Kaizer wakiona kama kocha huyo Muargentina anaweza kuja kuwa suluhisho la kusitisha ufalme wa Mamelodi katika Ligi ya PSL.

“Bado viongozi wa juu hawajafanya maamuzi ya mwisho inaweza kuwa Nabi au Gamondi, kitu pekee kwa Gamondi ni namna alivyowazuia Mamelodi unajua hii miaka ya karibuni ndio wamekuwa wakichukua ubingwa mfululizo,” alisema mmoja wa mabosi wa juu wa klabu hiyo ya Kaizer aliyepo kitengo cha ufundi.

“Unajua Gamondi analijua soka la hapa na amekaa Mamelodi, lakini uthubutu alioufanya mbele ya timu yake ya zamani umewafanya watu wa hapa washtuke hakuna aliyetarajia kile kiwango, nadhani hata nyie huko Tanzania mlidhani Yanga ingepoteza vibaya na yote yamewezekana kwa mbinu zake.”

Hatua ya kushtua zaidi kwa Yanga ni Gamondi mkataba wake na Yanga umebakiza miezi tu kabla ya kumalizika mwisho wa msimu huu, kitu kilichowaongezea mzuka mabosi wa Kaizer kuliweka jina lake mezani.

Kama mnakumbuka wakati Yanga inarejea kutoka Afrika Kusini, Gamondi alishtua zaidi alipozungumza na  kusema bado hana uhakika kama ataendelea na Yanga kwa msimu ujao, kauli iliyoongeza presha kwenye mustakabali wa kocha huyo klabuni hapo.

Ndani ya msimu huu, Gamondi ameiongoza Yanga kuweka rekodi ya kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku pia akiibakisha timu yake kwenye ramani ya ubingwa Yanga ikishinda mechi 17 kati ya 20 ilizocheza, huku akiwa ameingiza timu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho (FA).

Kocha huyo alimpokea Nabi, baada ya Mtunisia kuipa Yanga mataji sita tofauti katika mkataba wake wa miaka miwili na nusu, akibeba Ligi Kuu mara mbili, Kombe la Shirikisho mara mbili na Ngao ya Jamii pia mara pili ambayo hata hivyo kwa sasa imeshanyakuliwa na Simba baada ya kuifunga Yanga kwa penalti jijini Tanga.

SOMA NA HII  BAADA YA KUIONA YANGA IKICHEZA JUZI..ZAHERA AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA...