Home Habari za michezo SAA KADHAA KABLA YA KUKIWASHA NA SIMBA…NABI ANUSA HATARI YA KIPIGO…ABADILI GIA...

SAA KADHAA KABLA YA KUKIWASHA NA SIMBA…NABI ANUSA HATARI YA KIPIGO…ABADILI GIA ANGANI CHAP…


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amepanga kubadilisha mbinu dhidi ya Simba kutokana na ubora wa watani wao hao wa jadi.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya Yanga kuingia kambini mapema wiki hii kujiandaa na mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Nabi alisema katika mchezo huo, wanakwenda kukutana na timu kubwa, hivyo ni lazima wacheze kwa kuwaheshimu ili wapate matokeo mazuri.

Nabi alisema Simba ina wachezaji wengi wa kimataifa ambao ni bora kama ukifanya makosa, basi lazima watakuadhibu.

Aliongeza kuwa, katika mchezo huo wataingia tofauti kwa maana ya kimbinu na mfumo watakaoutumia ambao ni wa kucheza kwa kuiheshimu Simba.

“Tulivyocheza michezo iliyopita ya ligi dhidi ya Namungo na KMC ni tofauti tutakavyocheza dhidi ya Simba, hivyo ni lazima tuingie uwanjani kwa mbinu tofauti za kuwaheshimu zaidi.

“Simba ina wachezaji wengi wa kimataifa ambao ni bora na wana uzoefu wa kupata matokeo mazuri, hivyo hatutaki kupoteza mchezo huu, ni lazima tubadilike kidogo.

“Simba ni kati ya kubwa katika ukanda huu wa Afrika, hivyo ni lazima ucheze nao kwa heshima ili kupata matokeo mazuri ambayo sisi tunayahitaji kwani tumekubaliana na wachezaji kupambana ili kufanikisha malengo,” alisema Nabi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTUNGULIWA KIMOJA DAR...WYDAD WAAMUA KUFANYA MAAMUZI HAYA MAZITO...