Home Habari za michezo UTAMU WA KLOPP WAUPAGAWISHA UONGOZI LIVERPOOL….WAAMUA LIWALO NA LIWE…

UTAMU WA KLOPP WAUPAGAWISHA UONGOZI LIVERPOOL….WAAMUA LIWALO NA LIWE…


Imeripotiwa kuwa Klabu ya Liverpool ipo kwenye mchakato wa kuanza mazungumzo na kocha wake, Jurgen Klopp kwa ajili ya kumuongeza mkataba mwingine wa kuendelea kusalia hapo baada ya huu wa sasa kubakisha miaka miwili.

Awali, Klopp raia wa Ujerumani alieleza dhamira yake ya kutaka kuachia ngazi baada ya kumalizika kwa mkataba wake huu wa sasa uliokuwa unaisha 2024, lakini yeye mwenyewe sasa ameonesha nia ya kutaka kuendelea kukinoa kikosi hicho na Liverpool wako tayari kumaliza suala hilo.

Klopp ambaye ameitoa klabu hiyo ‘shimoni’ mpaka kuwa tishio England na Ulaya, mpaka sasa msimu huu amefanikisha Majogoo hao kutwaa ubingwa wa Kombe la Carabao, huku ikiwa hatua ya fainali ya Kombe la FA.

Pia Liverpool jana ilishinda mchezo wake wa nusu fainali ya kwanza ya Klabu Bingwa Ulaya ikiitungua Villarreal mabao 2-0 wakati kwenye Ligi Kuu England ikiendelea kupambania ubingwa wakiwa nafasi ya pili kwa pointi 79 dhidi ya pointi 80 za vinara Manchester City.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA ZORAN ALIVYOWAPELEKA PUTA SIMBA...AZAM FC WAAMUA KUMPA UKWELI HUU MAPEMA KOCHA WAO MPYA...