Home Habari za michezo KIMENUKAAH…WASAUZI WAISHITAKI SIMBA CAF KWA KUCHOMA UWANJA WAO MOTO…

KIMENUKAAH…WASAUZI WAISHITAKI SIMBA CAF KWA KUCHOMA UWANJA WAO MOTO…


MTENDAJI MKUU wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchini Afrika Kusini Tebogo Motlanthe amesema kitendo cha Klabu ya Simba kutoka Tanzania kuchoma kitu katikati ya Uwanja ni jambo la aibu na si la kiuanamichezo.

Motlanthe amesema kitendo hicho hakikubaliki na tayari kama Shirikisho tayari wameandika barua kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuona hatua stahiki zinachukuliwa.

Klabu ya Simba ilitolewa na Klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-3 baada ya timu hizo kufungana bao 1-1 katika michezo yote miwili ya hatua hiyo ya mtoano.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA ALIA NA FREDY & MUKWALA