Home Habari za Simba Leo KOCHA SIMBA ALIA NA FREDY & MUKWALA

KOCHA SIMBA ALIA NA FREDY & MUKWALA

Habari za Simba-

KOCHA Mkuu wa Simba Fadlu Davids ameelezea namna ambavyo anaumizwa na washambuliaji wa timu yake kutotumia nafasi, ambazo tiu inazitengeneza na kuzigeuza kuwa magoli.

Licha ya kikosi chake kuibuka na ushindi kwenye mechi mbili mfululizo za kirafiki, Fadlu amelia na washambuliaji kushindwa kutumia nafasi.

Simba ilianza kucheza na Canal SC ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 na juzi Jumapili ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Telecom Egypt. Jana ilikuwa na kibarua cha kukabiliana na Al-Adalah FC kutoka nchini Saudi Arabia.

“Hadi sasa nimewini maeneo mawili kuanzia utimamu na kuwajenga kisaikolojia, shida iliyopo ni namna ya kutumia nafasi tu lakini hilo sio gumu kwani kama wanaweza kutengeneza kutumia ni suala la muda,” alisema na kuongeza.

“Wamekuwa wakitengeneza nafasi nyingi lakini wanashindwa kutumia hilo halinipi shida sana kwani licha ya kuzikosa bado wanakuwa kwenye maeneo sahihi kupambana.

“Timu imeimarika kila eneo na wachezaji tayari wameanza kuingia kwenye mfumo, shida ya kutofunga ni sehemu ndogo ambayo inaweza kuisha kwa muda mfupi kwani wachezaji wamekuwa wakijitenga vizuri kwenye nafasi.” Alisema Fadlu Davids Kocha Mkuu wa

Kocha huyo ambaye ametua Simba kuchukua nafasi ya Abdelhak Benchikha, amesema kwa muda waliokaa Misri tayari ameshuhudia mabadiliko makubwa kikosini na anaamini hadi wakirudi Dar, atakuwa amejenga kikosi bora.

Simba Day kitaeleweka na Ligi ikianza kila kitu kijulikana.

SOMA NA HII  YANGA WAZIDI KUIMARISHA KIKOSI...WASHUSHA MASHINE HATARI..MAKOCHA AFRIKA WAIOGOPA SIMBA...