Home Habari za Simba Leo SIMBA YAFICHA SILAHA ZAKE…FADLU AONGEZA MBINU

SIMBA YAFICHA SILAHA ZAKE…FADLU AONGEZA MBINU

HABARI ZA SIMBA- FADLU

MNYAMA Aisseh ana Balaa huyo. Wanafahamu kwamba wapinzani wao wa jadi, Yanga watakutana nao Agosti 8 kwenye Ngao ya Jamii, wakaamua kufanya sapraizi ambayo wanaamini itawalipa.

Simba ambao wanatimiza wiki ya tatu kamili tangu waanze mazoezi katika kambi nchini Misri, wakiwa huko wamepata akili mpya kuelekea Simba Day ambayo itafanyika siku tano kabla ya kucheza dhidi ya Yanga.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika kambi yao iliyopo Mji wa Ismailia nchini Misri, benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids wameziba mianya kuanzia kambini hadi mazoezini hawataki kuona siri zao nyingi za ndani zikivuja.

Mtoa taarifa huyo amebainisha kwamba, usiri unaofanyika kambini ni katika kuhakikisha wanajenga kikosi kitakachofanya vizuri msimu ujao kwa kuanza na ushindi Kariakoo Dabi.

“Kuna usiri mkubwa sana kambini, ndiyo maana unaona mpaka sasa watu wengi hawafahamu ishu nyingi zinazoendelea huku kambini.

“Viongozi wameamua kufanya hivyo kwa sababu kocha amehitaji ili wachezaji kuwa na utulivu unaotakiwa kipindi cha kujiandaa na msimu,” alisema mtoa taarifa huyo.

Sapraizi Kubwa kwa Yanga

Habari zinabainisha kwamba, Simba kuficha silaha zao hawataishia kambini Misri pekee, bali hata wakirejea Dar es Salaam mwendo utakuwa ni uleule.

Mtoa taarifa huyo aliendelea kubainisha kwamba, hata katika mechi ya Simba Day, kocha atafanya ujanja ambao wapinzani wakiangalia mechi hawawezi kupata kitu cha maana sana.

“Timu ikirejea Dar Jumatano, itaendelea na kambi kama kawaida ikiwa kwenye uangalizi maalum, hali hiyo itaendelea hadi tutakapocheza Ngao ya Jamii.

“Hii yote ni katika kuelekea kusaka matokeo mazuri dhidi ya wapinzani wetu kwenye mechi za kimashindano.

“Tunafahamu kwamba tuna mechi ya kirafiki katika Simba Day na mashabiki wetu wanataka kuwaona wachezaji wao. Wasijali watawaona lakini itakuwa tofauti.

“Unajua mpaka sasa kocha tayari ana kikosi chake cha kwanza, hiyo siku ya mechi katika Simba Day atawachanganya lakini anaweza kuwapa muda mchache wa kucheza ili kulinda wasiumie,” alifichua mtoa taarifa huyo.

SOMA NA HII  BAADA YA 'KUIBANJUA KIMOKO' NAMUNGO...MGUNDA AFUNGUKA YA MOYONI SIMBA..