Home news BAADA YA KUWA MAJERUHI KWA MUDA MREFU…UONGOZI YANGA WAJA NA HILI KUHUSU...

BAADA YA KUWA MAJERUHI KWA MUDA MREFU…UONGOZI YANGA WAJA NA HILI KUHUSU YACOUBA…

 


KIUNGO wa Yanga, Yacouba Songne, yupo kwenye hatua za mwisho za kuimarika afya yake kabla ya kuungana na timu na kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).

Yacouba kwa sasa yupo kwenye program maalumu chini ya kocha wa viungo ambayo inamrejesha taratibu kwenye hali yake ya kawaida na huenda wiki ijayo ataungana na wenzake katika viwanja vya mazoezi.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabity Kandoro, alisema kuwa alikuwepo kwenye uwanja wa mazoezi juzi na aliona namna ambavyo Yacouba anatia matumaini na anaonyesha amebakiza siku chache ili aweze kurejea uwanjani.

“Yacouba huenda wiki ijayo akaanza mazoezi ya uwanjani, kwa maana nilivyomuona juzi anaonekana hana muda mrefu. Kwa sasa yupo chini ya program ya kocha wa viungo na huenda wiki ijayo akaungana na wenzake,” alisema.

Yacouba yupo nje ya uwanja kwa muda sasa akiuguza majeraha ya goti ambayo aliyapata kwenye mechi ya ligi na kulazimika kufanyiwa upasuaji.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA YANGA AKABIDHIWA MIKATABA YA MNATA, SHIKALO