Home Habari za michezo PAMOJA NA USHINDI WA GOLI 4-0 JUZI…NABI AFURA KWA HASIRA NAMNA MAYELE...

PAMOJA NA USHINDI WA GOLI 4-0 JUZI…NABI AFURA KWA HASIRA NAMNA MAYELE NA AZIZI KI WALIVYOCHEZA….


Yanga juzi jioni ilipata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Zalan ya Sudan Kusini katika mecchi ya kwanza ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikishuhudia Fiston Mayele akiweka rekodi kwa kufunga hat trick, ila kocha Nasreddine Nabi amegeuka mbogo na kuwapiga mkwara nyota wake.

Nabi amewajia juu nyota wake hao akitaka wajitathimini haraka kabla ya mechi ya marudiano ya ligi hiyo ya CAF akisema kwenye mchezo wa kwanza asilimia kubwa walicheza ovyo licha ya ushindi huo.

Akizungumza Nabi alisema licha ya ushindi huo, lakini wachezaji wake wamuamuacha na simanzi jinsi walivyopoteza nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza ambacho kilimalizika kwa 0-0.

Ushindi huo wa Yanga ulitengenezwa katika dakika 45 za kipindi cha pili shujaa akiwa Mayele aliyefunga hat- trick, kiliyokuwa ya kwanza kwake tangu ajiunge na Yanga, lakini akiwa mchezaji pekee kwa mechi za CAF zilizochezwa juzi na kufikia pia rekodi iliyowahi kuweka na Mrisho Ngassa mara mbili msimu wa 2009 na 2014 alipofunga jumla ya hat trick tatu dhidi ya Etoile d’Or na Komorozine za Comoro.

Pia kumfikia Boniface Ambani kwa nyota wa kigeni kutoka klabu ya Tanzania kufunga hat trick katika Ligi ya Mabingwa, alipofunga dhidi ya Etoile d’Or 2009, japo Kipre Tchetche naye akiwa Azam alifunga mabao matatu katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2016 dhidi ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini.

Bao jingine la Yanga juzi liliwekwa kimiani na kiungo fundi, Feisal Salum ‘Fei Toto’, lakini Nabi alisema wachezaji wake walioanza dakika 45 za kwanza wanatakiwa wajitathimini kwa kushindwa kuwa na utulivu katika kufunga kupitia nafasi nyingi ambazo walitengeneza.

Waliocheza kwenye muda huo ni pamoja na Stephane Aziz KI, Dickson Ambundo, Jesus Moloko, Mayele na Fei Toto kabla ya kocha Nabi kufanya mabadiliko baadaye kipindi cha pili na timu kupata mabao hayo yaliyowaweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu raundi ya kwanza kama itapata japo sare Jumamosi hii watakaporudiana na Wasudan.

SOMA NA HII  HUYU HAPA KIUNGO MCONGO 'MKATA UMEME' ANAYEZIGOMBANISHA SIMBA NA YANGA..ISHU NZIMA IKO HIVI..

“Haya ni mashindano ambayo unahitajika sana kutumia nafasi ambazo unatengeneza, nafahamu huwezi kufunga katika kila nafasi, ila ilikuwa aibu kubwa kwenye zile dakika 45 za kwanza,” alisema Nabi.

“Ingewezekana tungeshinda mabao mengi zaidi, nafahamu kwamba tupo kwenye ti8mu ambayo ina presha ya matokeo, lakini kama mchezaji lazima uwe na utulivu unapofika lango la wapinzani,ukivaa jezi ya Yanga lazima ucheze kwa akili kubwa.

Kocha huyo aliongeza kuwa licha ya kushinda hivyo bado wana kazi kubwa katika kusuka timu hiyo kuekekea mchezo wa marudiano baina ya timu hizo.

“Tuna kazi kubwa bado huu sio ushindi ambao utatufanya tuone tumeimarika, tunatakiwa kucheza kwa ubora mkubwa zaidi, tutayafanyia kazi haya katika mazoezi yetu kabla ya mchezo ujao.”

Timu hizo zitarudiana wikiendi ijayo Septemba 17 kwenye uwanja huo huo ambapo Yanga sasa itarejea kama timu mwenyeji wakiwa na faida ya ushindi kutoka mchezo wa kwanza.