Home Ligi Kuu RUVU SHOOTING YAIPIGIA HESABU TANO BORA

RUVU SHOOTING YAIPIGIA HESABU TANO BORA


 UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa unahitaji kumaliza ligi kwa msimu ujao ndani ya tano bora kwa kuwa mpango wao kazi kwa msimu wa 2020/21 ulibuma.

Ikiwa inanolewa na Kocha Mkuu, Charles Mkwasa ilimaliza ikiwa nafasi ya 11 na pointi zake ni 41 kibindoni.Hesabu zao ndefu kwa msimu ujao ni kuona inamaliza ndani ya nafasi za juu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema kuwa walipokosea wanapajua na watapambana kuwa tofauti katika msimu mpya.

“Msimu uliopita ipo sehemu ambayo tulikosea na tunajua hivyo msimu ujao tutakuja katika hali ya utofauti na kufanya vizuri katika kufikia malengo yetu na tunapambana kufikia ndani ya tano bora.

“Maandalizi yapo vizuri na kila kitu kinakwenda sawa ikiwa ni pamoja na kuona tunafanya vizuri kwenye mashindano ambayo tutashiriki msimu ujao,” alisema Bwire.

SOMA NA HII  MAXIME : TUMEACHANA NA KAGERA SUGAR..KAMA KUNA TIMU INANITAKA IJE..!!