Home Uncategorized DUA MAALUM AFANYIWA MBWANA SAMATTA

DUA MAALUM AFANYIWA MBWANA SAMATTA


FAMILIA ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, juzi usiku ilikutana na kusoma dua ya kumtakia kheri kijana wao katika harakati za kuanza kucheza Ligi Kuu England.

Samatta ameendelea kugonga vyombo mbalimbali vya habari duniani kufuatia taarifa za uhamisho wake wa kwenda Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England akitokea KRC Genk ya Ubelgiji.

Baba mzazi wa mshambuliaji huyo, Mzee Ally Samatta, amesema ilikuwa kawaida yake kumuombea dua mwanaye kila anapokuwa anapiga hatua moja kwenda nyingine, lakini awamu hii wameamua kuifanya kifamilia zaidi kwa kuwa hatua ambayo mtoto wao amefi kia ni kubwa sana.

“Imekuwa kawaida nyangu kumuombea dua kijana wangu kila anapokuwa anapiga hatua moja kwenda nyingine, lakini safari hii imekuwa ni hatua kubwa sana, kwa sababu anakwenda kwenye ligi ambayo alikuwa anaota kucheza tangu akiwa mdogo, hivyo tumeamua kukutana wanafamilia na kuangusha dua, ili Mungu aweze kumpa nguvu na uwezo wa kufanya vizuri kwenye klabu hiyo,” alisema Mzee Samatta.
SOMA NA HII  RASMI UWANJA WA TAIFA WABADILISHWA JINA SASA KUITWA UWANJA WA BENJAMIN MKAPA