Home Uncategorized MZIMU WA MAJERUHI WAITESA UNITED, SASA YAHAHA KUMTAFUTA MBADALA WA RASHFORD

MZIMU WA MAJERUHI WAITESA UNITED, SASA YAHAHA KUMTAFUTA MBADALA WA RASHFORD


OLE Gunnar Solskajer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa anafanya mpango wa kumtafuta mbadala wa Marcus Rashford kwa mkopo baada ya kuthibisha kwamba nyota huyo hatakuwa ndani ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu.
Nyota huyo mwenye mabao 14 ndani ya Ligi Kuu England aliukosa mchezo wa jana dhidi ya Liverpool uliochezwa Uwanja wa Anfield kutokana na kusumbuliwa na majeraha na United ilichapwa mabao 2-0.
Solkajaer amesema: “Ni lazima kwetu tuangalie namna gani tunaweza kumpata mchezaji ambaye tutampa dili hata la muda mfupi kwa ajili ya kuwa nasi kwenye msimu huu unaoendelea kwa sasa.
“Kwa sasa tunatazama namba na kiasi kamili ambacho kinahitajika kama itakuwa ni kumnunua jumla sawa hata ikiwa kwa mkopo hatuna tatizo katika hilo tutafanya ili kuona ni namna gani tutaendelea kupambana.
“Ni bahati mbaya kwetu kwa sasa tuna majeruhi wengi na wachezaji muhimu ambao ni pamoja na  Marcus, Anthony (Martial), Paul (Pogba), Scott (McTominay hawa wote ni majeruhi,” amesema.
SOMA NA HII  POLISI TANZANIA YAPANIA KUPAMBANA TPL