Home Uncategorized KOCHA SIMBA KUIBUKIA TIMU NYINGINE LIGI KUU

KOCHA SIMBA KUIBUKIA TIMU NYINGINE LIGI KUU


KMC ambayo imepata nafasi ya dezo ya kushiriki Kombe la Shirikisho msimu ujao iko kwenye mazungumzo na Kocha wa zamani wa Simba na sasa Lipuli, Seleman Matola.

Dili hilo limeanza baada ya KMC kushtukia kwamba Kocha wao wa sasa Etiene Ndayiragije huenda akatua Azam muda wowote.

Habari zinasema kwamba Ndayiragije ambaye ni Mrundi amefikia pazuri na Azam lakini mambo yanakwenda kimyakimya.

Viongozi wa KMC nao wakaamua kujiongeza na kumuita Matola mezani na habari zinasema kwamba mambo yako vizuri na huenda dili likatiki freshi kabisa.

KMC wameukubali uwezo wa Matola lakini habari zinasema kwamba watalazimika kutafuta Kocha mwingine ambaye atasaidiana na Matola kwenye michuano ya kimataifa kwani yeye hana leseni kubwa.

Matola hana mkataba na Lipuli baada ya Ligi Kuu Bara kumalizika.

SOMA NA HII  CHEKI NAMNA MAKUNDI YA AFCON MWAKA 2021 YALIVYO, TANZANIA SAHANI MOJA NA WAARABU