Home Habari za michezo POLISI TZ WAIKALIA YANGA KOONI KUELEKEA MECHI YA KWANZA YA LIGI KUU…WAKUMBUSHIA...

POLISI TZ WAIKALIA YANGA KOONI KUELEKEA MECHI YA KWANZA YA LIGI KUU…WAKUMBUSHIA KIPIGO CHA VIPERS…


Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Joslin Sharif amesema kuwa kuelekea mchezo wao wa kwanza wa ligi dhidi ya Yanga watatumia mchezo wa kirafiki na wapinzani wao dhidi ya Vipers kwa ajili ya kupata ushindi.

Polisi wanatarajia kuanza ligi kwa kumenyana na Yanga Agosti 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Amri Abeid, Arusha.

Kocha Joslin amesema kuwa “Tunamshukuru Mungu timu ipo sawa tuko tunajiandaa na mchezo wetu dhidi ya Yanga.

“Tunatarajia kurudi Moshi kesho, nimeona Yanga wana timu nzuri ila tutapambana kama wanaume kwani nilishuhudia mchezo wao dhidi ya Vipers hivyo nimeona namna wanavyocheza nitatumia mbinu zile kwa ajili ya kupata ushindi.”

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA MAN UTD KUMTEMA...WAZIRI SAUDI ARABIA AAGIZA RONALDO ASAJILIWE KWAO..