Home Habari za michezo WAKATI LIGI IMESIMAMA….MAKOCHA LIGU KUU WAIBUKA NA MISIMAMO YAO YA KIBABE….WAIGOMEA TFF...

WAKATI LIGI IMESIMAMA….MAKOCHA LIGU KUU WAIBUKA NA MISIMAMO YAO YA KIBABE….WAIGOMEA TFF MPAKA KIELEWEKE….


Hakuna kupoa, hivyo ndivyo unavyoweza kusema kutokana na timu zote 16 za Ligi Kuu Bara kuendelea na maandalizi katika wiki mbili za kupisha mechi za Timu za Taifa kufuzu CHAN, Tanzania ikicheza na Uganda.

Makocha wa timu hizo wamesema michezo miwili waliyocheza wameona ubora na mapungufu ya timu zao, hivyo wataendelea na maandalizi kama ili kuimarisha vikosi.

Mabingwa watetezi Yanga, Simba, Azam FC, Geita Gold ambao ni wawakilishi kwenye mashindano ya kimataifa wamesema hakuna cha kupoteza wanahitaji uimara zaidi ili waweze kutoa ushindani.

Wakati wawakilishi hao wakifunguka hayo timu nyingine 12 zinazoshiriki ligi makocha wake wamesema wanahitaji kuendelea na kambi kama kawaida.

Kocha Nasreddin Nabi, “Timu haikuwa na maandalizi mazuri, hivyo tunaendelea pale tulipoishia leo tunaanzia Gym mara baada ya wachezaji kupewa siku mbili za mapumziko.”

Zoran Maki alisema anawahitaji wachezaji wake kambini leo ili waendelee kukiimarisha kikosi chao huku timu hiyo ikiwa na mwaliko maalum nchini Sudan na timu ya Al Hilal ambapo itakuwa na mechi za kirafiki kujiweka fiti.

Kocha wa Geita Gold Freddy Felix ‘Minziro’ alisema ana kila sababu ya kuendelea kubaki na wachezaji wake kutokana na mashindano makubwa yaliyo mbele.

Kocha wa Azam, Abdihamid Moallin, alisema timu imeendelea na kambi na ana mpango wa kucheza mechi za kirafiki ili kuboresha upungufu.

Wakati wawakilishi hao kwenye mashindano ya kimataifa wakifunguka hayo Kocha wa Singida United, Hans Pluijm alisema wanaenda Mwanza kujiweka fiti tayari kwa mechi yao ijayo dhidi ya Dodoma Jiji.

Kocha wa Ihefu FC, Zuber Katwila alisema hawana mapumziko wanaendelea na maandalizi kwaajili ya kuboresha pale upungufu.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA ONANA KUTAKIWA NA WAALGERIA....SIMBA WAIBUKA NA TAMKO HILI RASMI...