BONDIA Mtanzania Hassan Mwakinyo ameomba msamaha kwa kushindwa dhidi ya mpinzani wake Liam Smith ambalo lilifanyika jijini Liverpool nchini Uingereza na Mwakinyo kushindwa kwa TKO.
Kushinwa kwa Mwakinyo ambaye alikuwa anaipeperusha bendera ya Tanzania kulifanya maamuzi ya mchezo huo yakawa ni kumtangaza Liam Smith kama mshindi wa pambano hilo.
Mwakinyo amemwaga machozi wakati alipokuwa akiwaomba msamaha Watanzania wote baada ya kupoteza pambano lake kwa TKO dhidi ya mpinzani bondia Smith, raia wa Uingereza katika pambano lililopigwa Septemba 3, 2022 ukumbi wa M&S Bank Arena uliopo jijini Liverpool nchini Uingereza.
Mbali na kuomba msamaha, Mwakinyo ameendelea kutoa maelezo juu ya kitu ambacho kilimpelekea kupoteza pambano hilo huku akisema kwamba uko uwezekano wa kufanyika kwa pambano la marudiano na bondia huyo kwa kile alichokieleza kwamba bado anaamini anao uwezo wa kumshinda bondia huyo kutoka nchini Uingereza Smith.
“Najua nimewaamuzi wengi nami pia sipendi kupoteza katika maisha yangu, nilibadilishiwa vifaa siku ya pambano kwa kuwa nilipewa viatu ambavyo sijawahi kufanyia mazoezi jambo ambalo lilinifanya nimwambie mwamuzi kuwa nina maumivu kwenye enka.
“Mara ya pili ilikuwa hivyo lakini mwamuzi hakuweza kunisikiliza na kuamua kumpa ushindi mpinzani wangu, sijapenda katika hili ninaomba msamaha,” amesema Mwakinyo