Habari za michezo

BAADA YA ‘KUBONDWA’ NA ZAMBIA JUZI….TWIGA STARS WARUDI KWA HASIRA…’WAIFUMUA’ MALAWI BILA HURUMA…

admin September 12, 2022 2:52 am


Baada ya kupata maumivu ya kupokonywa ubingwa na Zambia kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Cosafa, hatimaye timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ imejifuta machozi ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namibia na kumaliza nafasi ya tatu.

Katika michuano hiyo inayoendelea nchini Afrika ya Kusini, Tanzania ilishiriki kama bingwa mtetezi baada ya kulichukua taji hilo mwaka jana.

Mchezo huo ambao ulianza saa 7:00 mchana kwa saa za Tanzania ndiyo ilikuwa yakwanza kuandika bao kupitia mkwaju wa faulo iliyopigwa na Christer Bahera dakika ya 12 kabla ya Aisha Juma kuisawazishia Namibia kwa kujifunga mwenyewe dakika ya 20, wakati anajaribu kuokoa mpira wa krosi iliyopigwa na Zenatha Coleman na kufanya kipindi cha kwanza kimalizike

Mabadiliko ya kipindi chapili kuingia kwa Enekia Kasonga, Mwanahamisi Omary na Diana Msewa yalichangia kuongeza kasi kwenye eneo la ushambuliaji la Twiga na dakika ya 88, krosi iliyopigwa na Mwanahamisi ilitua kwenye boksi la Namibia na katika harakati za kuokoa kapteni Emma Naris akajikuta anaweza mpira nyavuni na kuipa Tanzania uongozi ambao ulidumu hadi mchezo unamalizika.

PAMOJA NA KUFUNGA ‘HAT-TRICK’ JUZI…MAYELE AKOLEZA MSIMAMO WAKE DHIDI YA YANGA KWENYE MECHI ZA CAF… PAMOJA NA SIMBA KUPATA USHINDI UGENINI…KUMBE JUMA MGUNDA ALIFANYA KAZI HII YA ZIADA KWENYE BENCHI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply