Habari za michezo

AHMED ALLY : TULIACHANA NA ZORAN KWA SABABU ALIKATAA BAADHI YA WACHEZAJI WETU…

admin September 16, 2022 12:15 pm


Msemaji wa Simba Ahmed Ally amesema miongoni mwa sababu ambazo ziliwafanya wasikie hatua ya kuachana na aliyekuwa Kocha wao Mkuu Zoran Maki ni kuwakataa baadhi ya wachezaji.

Ahmed ameyasema hayo Septemba 16, 2022 alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi TV akielezea maandalizi yao ya mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi ambapo alipoulizwa kuhusu sababu ya kuachana na Zoran ndipo aliposema sababu hiyo.

“Hiyo ya kuwakataa baadhi ya wachezaji ni miongoni mwa sababu ambayo ilitufanya tuachane na Zoran lakini kwa ujumla tulifikia mahali tukaona hatuwezi kwenda pamoja na Zoran, na yeye akaona hawezi kufanya kazi na Simba,” alisema Ahmed.

BAADA YA KISINDA KURUHUSIWA KUCHEZA LIGI KUU…JEMEDARI SAIDI AIBUKA NA KUTUPA KOMBORA HILI KWA TFF.. KIPA LIGI KUU ALIA KUDHALILISHWA NA SHUTI LA AZIZ KI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply