Home Habari za michezo BAADA YA KUONYESHA ‘MANJENJE’ YAO….MAYELE NA PHIRI WATABIRIWA VITA ….LUNYAMILA ATAJA BORA...

BAADA YA KUONYESHA ‘MANJENJE’ YAO….MAYELE NA PHIRI WATABIRIWA VITA ….LUNYAMILA ATAJA BORA KATI YAO…


Mastraika Moses Phiri wa Simba na Fiston Mayele (Yanga) kuna uwezekano mkubwa wakafunga mabao mengi msimu huu, kutokana na kasi waliyoanza nayo kwenye mashindano mbalimbali.

Nje na mechi za kirafiki ambazo timu zao zilicheza zikijiandaa na msimu mpya, Mayele amehusika katika mabao manane kwenye mechi tano za michuano yote akifunga saba na asisti moja katika Ngao ya Jamii (mabao mawili) aliyofunga dhidi ya Simba, Ligi Kuu Bara (mawili) na Ligi ya Mabingwa Afrika (matatu).

Mabao ya Ligi Kuu alifunga moja dhidi ya Coastal Union, Yanga ikishinda 2-0, la pili alitupia dhidi ya Polisi Tanzania katika ushindi wa 2-1.

Katika mechi ya CAF, Mayele alifunga hat-trick ya kipindi cha pili na kutoa asisti ya bao la nne la Feisal Salum waliposhinda 4-0 dhidi ya Zalan FC ya Sudan.

Mayele ndiye aliyekuwa kinara wa mabao 16 ndani ya Yanga na mfungaji namba mbili wa Ligi Kuu nyuma ya George Mpole wa Geita aliyechukua Kiatu cha Dhahabu msimu uliopita kwa mabao 17.

Phiri ambaye anacheza kwa mara ya kwanza nchini, amefunga bao katika mechi zote nne mfululizo za michuano yote alizocheza, akitupia matatu katika Ligi Kuu, ambako alianza katika ushindi wa Simba wa 3-0 dhidi ya Geita Gold, ushindi wa 2-0 dhidi ya Kagera Sugar na sare ya mabao 2-2 dhidi ya KMC.

Mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Simba ilikwenda kucheza Malawi dhidi ya Nyasa Big Bullets, ilishinda mabao 2-0, Phiri alitupia moja.

Phiri alilizungumzia hilo, kwamba anatamani kufunga sana na huduma yake iifae timu yake kupata ushindi.

“Ligi ni ngumu, lakini lazima tuonyeshe ushindani, ninachokitamani ni kufunga zaidi kuisaidia timu yangu, nikisaidiana na wachezaji wenzangu,” alisema Mzambia huyo.

Edibily Lunyamila, staa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, alisema mwanzo wa Mayele na Phiri unatoa taswira ya namna wanavyoweza wakawa na msimu mzuri wa kufunga idadi kubwa ya mabao, huku beki wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa akisema dalili njema huonekana asubuhi.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO...ZIMBWE Jr AVUNJA UKIMYA SIMBA...AFUNGUKA KUHUSU MAPUNGUFU YAO...