Habari za michezo

BAADA YA MALALAMIKO KUWA MENGI….HATIMAYE BODI LA LIGI WAIBUKA NA KAULI HII KWA WAAMUZI LIGI KUU…

admin September 16, 2022 12:29 pm


Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imesema baadhi ya waamuzi wanakosa ujasiri, kuwasiliana, mwendelezo na kutumia akili ya kuzaliwa wanapochezesha mechi mbalimbali hapa nchini na ofisi yake inawakumbusha ili mwamuzi awe bora ni lazima awe na vitu hivyo, imefahamika.

Akizungumza na Kamati ya Waamuzi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almasi Kasongo, alisema kumekuwa na malalamiko mengi kwa waamuzi lakini ikifuatiliwa inagundulika baadhi wanakosa sifa hizo alizozitaja.

“Mwamuzi ni kama hakimu au jaji, ni lazima kwanza uwe jasiri, na mwamuzi mzuri anapimwa kwa vitu kama hivyo.”

“Kuna baadhi ya waamuzi wamekariri penalti haitoki dakika ya 94, au dakika ya kwanza, huko ni kukosa ujasiri, penalti inatoka dakika yoyote ile hata dakika ya 97 na kadi nyekundu inatoka muda wowote ule na anaonyeshwa yoyote yule,” amesema Kasongo.

KIPA LIGI KUU ALIA KUDHALILISHWA NA SHUTI LA AZIZ KI… ISHU YA KAGERE NA WENZAKE KUANZA KWA ‘MGUU WA KUSHOTO’ SINGIDA….KOCHA WAO AVUNJA UKIMYA ..ATAJA CHANZO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply