Huyu Mwamba anaitwa Musa Noah Kamara amezaliwa August 06, 2000 maeneo ya Tombo, Sierra Leone jina lake maarufu ni Musa Tombo ni mshambuliaji hatari wa timu ya taifa ya Sierra Leone kijana ana kipaji hasa yupo chini ya wakala Roland Ekokobe.
Musa mwenye umri wa miaka 22 ameshidwa kabsa kucheza soka nje ya Sierra Leone sio kwa sababu ya kipaji ni kwa sababu zake mwenyewe mara ya kwanza alipelekwa Sweden kwenye klabu ya Trelleborgs FF baada ya kusajiliwa akakataa kwa kusema kuna baridi na kuanza kulia siku nzima siku ya pili wakala wake akamua kumrudisha nyumbani kwao Sierra Leone.
Musa ni mshambuliaji hatari sana kuna wakala mmoja alijitokeza na kumpeleka Norway kwenye timu ya ligi kuu alisajiliwa bila hata kufanyiwa majaribio Musa baada ya kushinda siku moja akaanza kulia na kulalamika akitaka arudishwe kwao wakala akadai wamuache tu atazoea, Musa akaendelea kulia na akatishia kujinyonga iwapo hawatamrudisha kwao wakala huyo akamurudisha haraka kwao Sierra Leone.
Kijana huyu wakasema labda ameshindwa kucheza soka nje ya Afrika juzi kati alisajiliwa na klabu ya Al Ittihad Tripoli ya Libya ameenda kujiunga na klabu ya hiyo baada ya siku 6 tu ameomba kurejeshwa nyumbani kwao Sierra Leone kwa madai ya kuwa anasikia milio ya bastola usiku nchini Libya hivyo haoni usalama wa kutosha.
Musa Noah Kamara Tombo amevujisha video fupi akiwa ameshika panga akiwa anasema endapo atauliwa (atakufa) akiwa nchini Libya basi wakala wake Roland Ekokobe na mke wake (Hawa) wanastahili kushitakiwa na kubeba lawama zote kwani alikuwa amekata tiketi ya kurejea nyumbani kwao Sierra Leone wao waka i-cancel tiketi yake.
Huyu ndio Musa Tombo ambaye ameshindwa kucheza soka nje ya Sierra Leone.