Home Habari za michezo A-Z JINSI MZUNGU WA SIMBA ALIVYOPAPATUKA SUDANI JANA USIKU…AL HILAL WASHINDWA...

A-Z JINSI MZUNGU WA SIMBA ALIVYOPAPATUKA SUDANI JANA USIKU…AL HILAL WASHINDWA KULIPA DENI….


KIKOSI cha Simba kimepoteza mchezo wake wa pili wa kirafiki kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Al Hilal.

Mchezo wa jana ni wa pili kwa Simba kucheza ikiwa nchini Sudan ambapo ilialikwa kwenye mashindano maalumu yaliyoandaliwa na Klabu ya Al Hilal.

Katika mchezo wa kwanza Simba ilishinda mabao 4-2 dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana.

Bao pekee la ushindi kwa Al Hilal limefungwa na John Mano dakika ya 62 na kuwafanya Simba kupoteza mbele ya wenyeji wao.

Nyota Gadiel Michael alikwama kuyeyusha dakika 90 baada ya kupata maumivu na nafasi yake ilichukuliwa na Okwa huku mshambuliaji mzungu wa Simba Dejan akianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo.

Pamoja na kufungwa huko, bado Al Hilal wameshindwa kulipa deni la kufungwa magoli manne na Simba , ambapo walifungwa kwenye michuano kama hii iliyoandaliwa na Simba mwaka juzi.

SOMA NA HII  MASTAA SIMBA, YANGA WAIJAZIA MAMILIONI TFF...'ISHU' NZIMA IKO HIVI...