Home Uncategorized UNITED BADO HAWAJAMPOTEZEA SANCHO

UNITED BADO HAWAJAMPOTEZEA SANCHO

 


MANCHESTER United imesema kuwa itatumia nguvu kubwa kumpata nyota wa Borrusia Dortmund, Jadon Sancho ambaye inaelezwa kuwa yupo kwenye rada za mabosi hao.


Sarakasi za kuipata saini ya Sancho kuibukia Manchester United zimekuwa zikiripotiwa kukwama mara kwa mara ambapo United inaelezwa kuwa iligomea dau ambalo mabosi hao walitaja.


Dortmund inahitaji euro milioni 100 ili kumuachia nyota huyo kuibuka ndani ya Old Trafford.


Kocha Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar amesema kuwa kwa sasa ni ngumu kuweka wazi kuhusu masuala ya usajili ambapo mpango wa kusajili mabeki kwenye kichwa chake haupo.


“Bado kuna uhitaji sehemu kadhaa lakini kwa upande wa mabeki nina amini kwamba hawa waliopo watafanya vizuri,” amesema.

SOMA NA HII  MCHEZAJI UTURUKI AMUUA MTOTO, AJIPELEKA POLISI