Home Habari za michezo AHMED ALLY : TULIACHANA NA ZORAN KWA SABABU ALIKATAA BAADHI YA ...

AHMED ALLY : TULIACHANA NA ZORAN KWA SABABU ALIKATAA BAADHI YA WACHEZAJI WETU…


Msemaji wa Simba Ahmed Ally amesema miongoni mwa sababu ambazo ziliwafanya wasikie hatua ya kuachana na aliyekuwa Kocha wao Mkuu Zoran Maki ni kuwakataa baadhi ya wachezaji.

Ahmed ameyasema hayo Septemba 16, 2022 alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi TV akielezea maandalizi yao ya mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi ambapo alipoulizwa kuhusu sababu ya kuachana na Zoran ndipo aliposema sababu hiyo.

“Hiyo ya kuwakataa baadhi ya wachezaji ni miongoni mwa sababu ambayo ilitufanya tuachane na Zoran lakini kwa ujumla tulifikia mahali tukaona hatuwezi kwenda pamoja na Zoran, na yeye akaona hawezi kufanya kazi na Simba,” alisema Ahmed.

SOMA NA HII  AHMED ALLY:- "MTASHANGAA SANA.....KAZI NDIO KWAANZAAA INAANZA...."