Home Habari za michezo BAADA YA MAKI KUONDOKA ….SIMBA WAANIKA MUSTAKABALI WA ‘STRAIKA MZUNGU’…WADAI HALIPO KWENYE...

BAADA YA MAKI KUONDOKA ….SIMBA WAANIKA MUSTAKABALI WA ‘STRAIKA MZUNGU’…WADAI HALIPO KWENYE MAKUBALIANO…


Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally amesema straika Mzungu, Dejan ataendelea kuwepo klabuni hapo kwani hahusiani moja kwa moja na kocha Zoran Maki aliyefungashiwa virago mchana huu.

Akizungumza mara baada ya kufanya mkutano wa ajili ya mechi yao kesho dhidi ya KMC, Ahmed alisema, wamefikia makubaliano ya kuachana na kocha Mkuu pamoja na kocha wa viungo Sbai Karim na kocha makipa Mohamed Rachid ambao ndiyo wanahusiana.

“Package ya Zoran ilikuwa na kocha wa viungo na kocha wa makipa. Mtu pekee ambaye kocha alimpendekeza alikuwa ni Mohamed Outara ambaye naye pia atabakia maana usaji wake hauhusiani na kocha.

“Outara ni beki mzuri na tunaendelea kumhitaji ndani ya klabu na Dejan vilevile hahusiani na kocha Zoran hata kidogo,” alisema Ahmed.

SOMA NA HII  PACHA YA MUGALU NA BOCCO YAMKOSHA KOCHA SIMBA