Home Habari za michezo BILIONEA WA CHELSEA AJILIPUA KWA KOCHA MPYA….AMPA MKATABA AMBAO HAKUNA KLABU YA...

BILIONEA WA CHELSEA AJILIPUA KWA KOCHA MPYA….AMPA MKATABA AMBAO HAKUNA KLABU YA EPL INGEWEZA KUFANYA…


THOMAS Tuchel alifutwa kazi ndani ya Klabu ya Chelsea baada ya kupoteza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Dinamo Zagreb.

Mbali na kichapo hicho pia Tuchel hakuwa na mwendo mzuri kwenye mechi za Ligi Kuu England msimu wa 2022/23.

Ni Graham Potter aliyekuwa Kocha Mkuu wa Brighton ametangazwa kuwa kocha mpya kwa dili la miaka mitano na alikutana na mmiliki wa Chelsea Todd Boehly siku ya Jumatano na kufanya naye mazungumzo.

Anakuwa ni kocha wa kwanza kupewa dili ndani ya Chelsea chini ya utawala wa mmiliki mpya wa timu hiyo ambaye amebainisha kuwa anatambua uwezo wake na wana imani naye.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO DHIDI YA YANGA....MABOSI SIMBA WAINGIA KITETE CHA KUPATA GUNDU KAMA LA MSIMU ULIOPITA...