Home Habari za michezo BREAKING NEWS:…JUMA MGUNDA KOCHA MPYA SIMBA…LESENI A YA CAF YAMPA ULAJI MBELE...

BREAKING NEWS:…JUMA MGUNDA KOCHA MPYA SIMBA…LESENI A YA CAF YAMPA ULAJI MBELE YA MATOLA NA MGOSI…


Klabu ya Simba Usiku huu imemtangaza Kocha Mkuu wa Coastal Union ya Tanga Juma Mgunda kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Katika taarifa ya Klabu hiyo kwa Mashabiki wake, Mgunda atasafiri na kikosi cha timu hiyo kwenda nchini Malawi ambapo Simba wataanza kampeni yao ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Hata hivyo taarifa hiyo haijabainisha wazi Mgunda amesaini mkataba wa muda gani, huku vyanzo vya karibu vikisema kuwa ameazimwa kutoka kwa timu yake maalumu kwa mechi hiyo huku Simba wakijipanga kutafuta Kocha Mkuu.

Aidha inaelezwa kuwa Mgunda amepata nafasi hiyo kutokana na kuwa na Leseni A ya CAF inayompa nafasi ya kuwa Kocha Mkuu kwenye mechi ya CAF huku uwezo wa kupandiha viwango vya wachezaji ikiwa ni sababu nyingine.

Kwa mantiki hiyo, Matola anaendelea kuwa Kocha Msaidizi, huku Mgunda akiwa kama Bosi wake mpaka pale itakavyotangazwa vingine.

Taarifa ya Simba Hii hapa chini.


SOMA NA HII  FIFA WAIBUKA NA HILI JIPYA SAKATA LA MABILIONI YA MSUVA KUTOKA KWA WAARABU....