Home Habari za michezo KISA USHINDI WA JANA MBELE YA PRISONS…MGUNDA AWAPIGA MKWARA SIMBA SC…ATAKA AHESHIMIWE….

KISA USHINDI WA JANA MBELE YA PRISONS…MGUNDA AWAPIGA MKWARA SIMBA SC…ATAKA AHESHIMIWE….


Kocha Mkuu wa muda Simba SC Juma Mgunda ametaja sababu za kumtoa Beki Henock Inonga Baka na kumpa nafasi Joash Onyango wakati wa mchezo wa Mzunguuko wanne wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Simba SC iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Maafande wa Tanzania Prisons jana Jumatano (Septemba 14), Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokione jijini Mbeya, bao likifungwa na Kiungo Jonas Gerard Mkude.

Mgunda amesema sababu kubwa ya kufanya mabadiliko ya kumtoa Inonga, ilitokana na Beki huyo kutoka DR Congo kupata majeraha ya misuli, hivyo alilazimika kufanya maamuzi hayo, ambayo amekiri hayakuwafurahisha Mashabiki wa Simba SC waliokua wanaufuatilia mchezo huo.

“Siku zote Mashabiki hupenda kile wanachokiona, lakini kiufundi Inonga alikua amepata majeraha ya misuli, ilinilazimu kumtoa na nafasi yake nikamuaru Joash Onyango akaitumikie.”

“Siwalaumu Mashabiki wanaoendelea kulaimu kwa mabadiliko hayo niliyoyafanya, lakini wanapaswa kuheshimu maamuzi ya kiufundi ambayo kwangu mimi kama Kocha yamenisaidia sana kwa kuzingatia afya ya mchezaji wangu ambaye bado ninamuhitaji kwa michezo inayofuata.” amesema Mgunda

Ushindi wa 1-0 unaiwezesha Simba SC kufikisha alama 10 sawa na Young Africans inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na uwiyano mzuri wa mabao ya Kufunga na Kufungwa, huku Azam FC ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 08.

SOMA NA HII  RASMI..MAGORI AVUNJA UKIMYA VITA YA BARBRA NA MANARA..AFUNGUKA KUHUSU UTAJIRI WA MO DEWJI