Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA CAF JUMAPILI…MASTAA SIMBA ‘WAPEWA VIDONGE VYAO’….YAWABOTSWANA MSIMU ULIPITA YATAJWA…

KUELEKEA MECHI YA CAF JUMAPILI…MASTAA SIMBA ‘WAPEWA VIDONGE VYAO’….YAWABOTSWANA MSIMU ULIPITA YATAJWA…


Klabu ya Simba imetoa shukrani kwa mashabiki na wadau wa timu hiyo waliosafiri nchini Malawi, huku ikiwaomba kujitokeza tena kwenye mechi ya marudiano na Nyasa Big Bullet Septemba 18 katika uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Simba ikicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi ya mabingwa Afrika mkondo wa kwanza hatua ya awali Septemba 10 katika uwanja wa Bingu jijini Lilongwe nchini Malawi na kushinda mabao 2-0 na Jumapili hii itakuwa kibaruani kuwakaribisha wapinzani hao.

Afisa Habari wa timu hiyo, Ahmed Ally amesema mafanikio ya Simba yanatokana na nguvu ya mashabiki kutokana na kuipambania kwa nguvu, ari na nia na kuwaomba kujitokeza tena kwa wingi kuujaza uwanja ili kuendeleza ushindi.

Kuhusu mechi ya jana ya Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons, Ally amekiri mambo yalikuwa magumu na kwamba wachezaji walipambana na kupata bao moja ambalo liliwahakikishia alama tatu muhimu.

“Kocha Mgunda na Msaidizi wake Seleman Matola wameshaongea na wachezaji, tunajua tulishinda mechi ya kwanza ugenini, ila hatuwezi kurudia yale yaliyojitokeza dhidi ya Jwaneng Galaxy, mashabiki tunaomba waje kwa wingi Jumapili kutupa nguvu,” amesema Ally

Msemaji huyo ameongeza kuwa uongozi unaendelea kuweka sawa mipango kuhakikisha wanafuzu hatua ya kwanza ya michuano hiyo na kubainisha kuwa watakuwa makini kuwakabili wapinzani hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Simba tawi la Nanenane jijini Mbeya, Benny Chacha amesema mashabiki wapo tayari kusafiri kwa ajili ya kuishangilia timu hiyo Jumapili na kwamba magari matano ainaya Coasta zimeshaandaliwa.

“Tunaanza safari Ijumaa hadi sasa Coasta nne zimejaa na leo moja itakuwa tayari kutokana na mwitikio ulivyo, niwaombe matawi mengine kujiandaa twende kuipa timu yetu sapoti ishinde na kusonga mbele,” amesema Chacha

Naye Katibu wa Simba mkoani Mbeya, Anold Nsekela amesema moto walioenda nao nchini Malawi na kuwazima wapinzani ndio huo huo wataenda nao Jumapili kuhakikisha timu inapata ushindi na kutamba kuwa Wana matumaini na chama lao kufanya kweli.

SOMA NA HII  GAMONDI HUYU ANATAKA KUFUATA NYAYO ZA MANARA!?

“Niwaombe mashabiki wengine kutoka matawi yote nchini twende kwa moto uleule Lupaso ili kuisapoti timu yetu, tunaamini mchezo huo Simba itashinda na kusonga mbele,” amesema Nsekela