Home Habari za michezo SAKATA LA MANARA KUFUNGIWA…TFF WAANZA KULEGEZA KAMBA MDOGO MDOGO…ISHU NZIMA IKO HIVI…

SAKATA LA MANARA KUFUNGIWA…TFF WAANZA KULEGEZA KAMBA MDOGO MDOGO…ISHU NZIMA IKO HIVI…


Msemaji wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Haji Sunday Ramadhan Manara amepunguziwa adhabu ya Faini kutoka Milioni 20 hadi Milioni 10, huku hukumu ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka miwili ikibaki palepale.

Maamuzi ya kumpounguzia adhabu Manara yametangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF Richard Mbaruku jana Jumatano (Septemba 14) majira ya Usiku.

Richard Mbaruku amesema Kamati yake imepitia Rufaa ya Haji manara na imeona haina mashiko lakini, lakini imelazimika kutumia busara kumpunguzia adhabu ya Faini.

Kamati ya Rufaa imemtaka Haji Manara kuhakikisha analipa faini hiyo ndani ya siku 30, baada ya kutangazwa kwa maamuzi ya Rufaa aliyoiwasilisha mbele yao.

July 21 Mwaka huu 2022, Haji Manara alitangazwa kufungiwa miaka miwili kujihusisha na soka pamoja na Faini ya milioni 20 baada ya kukutwa na hatia ya kumkosea nidhamu Rais wa TFF Wallace Karia wakati wa mchezo wa Fainali Kombe Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kati ya Young Africans dhidi ya Coastal Union, uliopigwa jijini Arusha July 02.

SOMA NA HII  YANGA KAMILI KUKWEA PIPA KUWAFUATA RIVERS UNITED