Home Uncategorized SIMBA QUEENS YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA PRINCESS

SIMBA QUEENS YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA PRINCESS


MUSA Mgosi, Kocha Mkuu wa timu ya Simba Queens amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya Dar Dabi ya Ligi ya Wanawake Tanzania, kesho Desemba 12 dhidi ya Yanga Princess. 


Yanga Princess kesho itakuwa ugenini Uwanja wa Simba Mo Arena kusaka pointi tatu ndani ya Ligi Kuu ya Wanawake ambayo imeanza kuwa na ushindani mkubwa.


Mgosi amesema:”Maandalizi yapo sawa na tunahitaji ushindi ili kuweza kufikia malengo tuliyojiwekea ya kutwaa ubingwa Kwenye  hii ligi ya Wanawake.


“Tunaamini mchezo utakuwa mgumu ila tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na tunatambua kwamba kwa kiasi fulani Yanga imeanza kuimarika tofauti na ile ya msimu uliopita.


“Yote kwa yote wachezaji wetu wana morali kubwa na nimewaambia kwamba tunahitaji ushindi katika mchezo huo wa kesho ninaamini itakuwa hivyo,”.


Mazoezi ya Simba Queens yanafanyika Kwenye Uwanja wa Toto Tundu uliopo Tabata Segera ambapo ipo kambi ya timu hiyo kwa sasa ambao ni mabingwa watetezi.

SOMA NA HII  NAMNA MORRISON NA MOLINGA WALIVYOWAFUNIKA WOTE BONGO - VIDEO