Home Uncategorized MUANGOLA WA YANGA HATIHATI KUKOSA MECHI ZOTE ZA MZUNGUKO WA KWANZA

MUANGOLA WA YANGA HATIHATI KUKOSA MECHI ZOTE ZA MZUNGUKO WA KWANZA

 


NYOTA wa Yanga, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ raia wa Angola yupo hatarini kukosa michezo yote mitatu iliyosalia ya raundi ya kwanza kutokana na majeraha ya nyonga aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Namungo.

Carlinhos mwenye mabao mawili na pasi mbili za mabao hapo awali alikuwa akisumbuliwa na jeraha la kisigino lililomfanya akose michezo mitano alirejea na kufunga bao kwenye mchezo dhidi ya Namungo Novemba 22, mwaka huu.

 

Baada ya kupona majeraha hayo, Carlinhos amepata majeraha ya nyonga ambayo yamemfanya akose michezo mitatu mfululizo dhidi ya Azam, JKT Tanzania na mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting.


Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija amesema: “Ni kweli mchezaji wetu, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ anaendelea na matibabu baada ya hivi karibuni kufanyiwa tena vipimo vya afya ambavyo vimeonyesha wazi bado afya yake haijatengemaa na ataendelea kuwa kwenye uangalizi wa madaktari.

 

“Mpaka sasa hatuna uhakika wa muda rasmi ambao atakuwa nje ya uwanja kwa sababu hii itategemea sana na kasi ya uponaji wa majeraha aliyonayo, lakini kuna uwezekano mkubwa akakosekana kwenye michezo mitatu iliyosalia ya mzunguko wa kwanza,” amesema Mngazija.


Chanzo: Championi

SOMA NA HII  VPL:YANGA O-0 MBEYA CITY