Home Habari za michezo SAKATA LA MKATABA WA GSM NA YANGA…JEMEDAR SAIDI AIZIDI KUFUKUNYUA MAMBO MAPYA…AANIKA...

SAKATA LA MKATABA WA GSM NA YANGA…JEMEDAR SAIDI AIZIDI KUFUKUNYUA MAMBO MAPYA…AANIKA YA NYUMA YA PAZIA..

Jana tulianzishiwa mada mahususi ambayo ilikuwa ya KIMKAKATI na vijana wakaiparamia kama ilivyo mwisho wa siku lengo likatimia.

Lengo lilikuwa ni kututoa njiani badala ya kujadili mambo ya msingi watu wakaingia kujadili mambo ya nini kijadiliwe na wachambuzi na kipi ni haramu.

Nimejiuliza ilikuwa ni bahati mbaya kwamba siku mkataba wa GSM & YANGA unatangazwa ndio siku hiyo hiyo tunaambiana tujikite kwenye dakika 90 na mengine tuyaache? Jibu baki nalo mwenyewe

Vijana kabla hamjaingia kwenye mada elekezi jaribuni kuona mitego kuizunguka hiyo mada. Ni kama swali unaloliona rahisi kwenye mtihani ukalivamia bila kujua kwamba lina mtego uliojificha, mwishowe unakwama.

Swipe hiyo video uone picha ya Wakurugenzi 2 wa GSM wakibadilishana mikataba kati ya Yanga na GSM.

Mkurugenzi wa Biashara wa GSM ALAN CHONJO na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM HERSI SAID, wakipozi kwa picha ya mkataba wa GSM na YANGA.

Kwa mtu ambaye anafikiri sawasawa hii inafikirisha sana vinginevyo kuna shida mahala. Najua Hersi ni Rais wa Yanga ndiyo, lakini hili kama wangekua smart enough wangeweza kumuweka Makamu wa Rais na au CEO kuwakilisha klabu.

Rais ndiye Chief Signatory wa klabu, lakini ndiye Mkuu wa kitengo cha uwekezaji wa Kampuni ya kazini kwake. Jamani hata hili nalo ni kwamba tunaichukia klabu? Jibu baki nalo mwenyewe.

Tukubaliane kwamba tunaweza kupishana kwenye kufikiri na wala hakuna chuki ila ni mitazamo tu.

BIN KAZUMARI (Voice Of The Voiceless)

SOMA NA HII  YANGA KILICHOWAPONZA NI DHARAU...MTAPIGWA NYINGI NA RIVERS