Home Habari za michezo BAADA YA BARCA KUBUGIZWA GOLI 3-1NA MADRID ….XAVI KAONA ISIWE TABU AISEE…KAAMUA...

BAADA YA BARCA KUBUGIZWA GOLI 3-1NA MADRID ….XAVI KAONA ISIWE TABU AISEE…KAAMUA KUTEMA ‘NYONGO’ MAZIMA…

Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi, amewaambia wachezaji wake wanahitaji kubadilika kama wanataka kushinda ubingwa wa La Liga msimu huu hiyo ni baada kupoteza mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid.

Kocha huyo wa klabu ya Barcelona ameoongea hayo baada ya kufungwa katika dimba la Santiago Bernabeu na Real Madrid kwa mabao 3-1 na kuwafanya Barcelona kuachia Uongozi wa Ligi hiyo ambayo walikua wanaongoza kwa tofauti ya magoli.

Xavi anawahitaji wachezaji wake kubadilika kuelekea michezo mingine kama kweli wana nia ya kua mabingwa wapya wa La liga msimu na kuupokonya ubingwa huo mikononi kwa Real Madrid ambao hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa msimu huu.

Gwiji huyo wa zamani wa klabu hiyo pia anaamini hawakutumia nafasi ambazo walizipata katika mchezo kitu ambacho wapinzani wao walikifanya kwa ufasaha na kuwafanya wao kutoka mikono mitupu katika mchezo huo.

Barcelona ya Xavi kwasasa inashika nafasi ya pili baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza msimu huu katika La liga lakini bado wana nafasi ya kufanya lolote msimu huu na kweza kuondoka na taji lolote.

SOMA NA HII  RASIMU YA KATIBA YAIGAWA SIMBA...RAGE APIGILIA MSUMBARI....