Home Habari za michezo FT: YANGA 1-1 SIMBA….AZIZ KI AKIMBIA NA FUKO LA MAMILIONI YA KINA...

FT: YANGA 1-1 SIMBA….AZIZ KI AKIMBIA NA FUKO LA MAMILIONI YA KINA OKRAH…

Dakika 90 za Dabi ya Kariakoo zinakamilika kwa sare ya goli 1-1 kati ya vigogo Yanga dhidi ya wekundu wa Msimbazi Simba SC.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam umeshuhudia nyota wapya ndani ya vikosi hivyo wakipachika magoli kwa kila upande.

Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa nyota wake Augustine Okrah dakika ya 15 akimaliza pasi safi ya Clatous Chama.

Stephen Aziz Ki akaisawazishia Yanga kwa mpira wa adhabu uliojaa wavuni na kumfanya Aishi Manula asijue la kufanya.

Kwa sare hiyo Simba anabaki kileleni ikiwa na alama 14 sawa sawa na Yanga waliopo nafasi ya pili huku Simba wakiwa na faida ya magoli ya kufunga.

SOMA NA HII  JUMATANO YA MAOKOTO YA MERIDIANBET IMEKUJA NA UHAKIKA WA ODDS HIZI ZA USHINDI...