Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA DABI KESHO…UKUTA WA SIMBA KIBOKO AISEE…TAKWIMU HIZI HAPA…

KUELEKEA MECHI YA DABI KESHO…UKUTA WA SIMBA KIBOKO AISEE…TAKWIMU HIZI HAPA…

Habari za Simba SC

Safu ya ulinzi ya Simba imekuwa ngumu kupitika kirahisi na katika mechi sita za kimashindano chini ya Kocha mkuu, Juma Mgunda akisaidiana na Seleman Matola, imeruhusu bao moja, huku safu ya ushambuliaji ikivuna mabao 12.

Ligi ya Mabingwa Afrika iliichapa Nyasa Big Bullets 4-0 nyumbani na ugenini na De Agosti mabao ya nyumbani na ugenini 4-1, wakati mechi za Ligi Kuu Bara iliifunga 1-0 Prisons na kuishushia kipigo cha mabao 3-0 Dodoma Jiji.

Mastaa wanaocheza nafasi ya ulinzi pale kati kuna Joash Onyango, Henock Inonga, Mohammed Ouattara, Kenney Juma na pembeni kuna Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Gadiel Michael, Shomari Kapombe na Israel Mwenda.

Pafomansi ilioonyeshwa na safu hiyo, imechambuliwa na mafundi wa zamani, wakidai Mgunda na Matola wamewaaminisha wachezaji hao wanaweza kufanya makubwa na imewasaidia kuwarejesha mchezoni.

Beki wa zamani wa Simba na Yanga, Amir Maftah alisema tofauti na msimu ulivyoanza, hakuwa anaiona kasi ya wachezaji, ila kwa sasa anaona wana mipango sahihi na kwa muda sahihi inayowafanikisha kushinda mechi.

“Simba ina kikosi kizuri isipokuwa wakati inaanza msimu huu wachezaji walikuwa na morali ya chini, jambo linaloonekana Mgunda na Matola wamewarejesha mchezoni, kila mmoja ana ari ya kufanya jukumu lake bila kusukumwa;

“Haina maana kama washambuliaji wanafunga, halafu ulinzi unakuwa uchochoro wa wapinzani kurudisha mabao, kinachofanyika ndani ya kikosi hicho kila nafasi inafanya jukumu lake inavyotakiwa.”

Mtazamo wake ulikwenda sambamba na wa beki wa zamani wa timu hiyo, Boniface Pawasa aliyesema, “Ni kitu kizuri, timu ikipata ushindi na mabeki wanaulinda, hilo wanapaswa kulizingatia zaidi hasa kwenye hatua ya makundi waliyotinga, kila mtu akafanye jukumu lake, asiwepo anayemtegea mwingine, maana kuna wakati mchezaji mmoja anakuwa anawajibika sana mwingine anapojisahau,” alisema.

SOMA NA HII  USHINDI WA YANGA ..NCHI NZIMA INASHEREKEA...MO DEWJI ASHINDWA KUJIZUIA ...